Leo Ndio Siku ya Tuzo za Muziki Tanzania za Kilimanjaro. (Tanzania Kili Music Awards 2011) Mimi na Band Yangu ya Mapacha Watatu (Jose Mara,Kalala Junior na Khalid Chokoraa) Tumefanikiwa Kuingia katika kinyang'anyiro Hicho Kwa category ya Wimbo Bora wa Kiswahili, Band. Pia Swahiba Wetu Khalid Chokoraa pia anagombea Rapa Bora wa Bendi. Kura Zimekwishakupigwa, tunaenda kuona sasa kama yaliyomo yamo.
MUHIMU ZAIDI NA FARAJA KWETU MAPACHA NI KUFANYA ONYESHO PALE KWENYE KILI AWARDS. AMBAO HAWAJAWAHI KUONA KAZI YETU BASI WATEGEMEE KUONA MUZIKI ULIO NA HESHIMA WA KIZAZI KIPYA CHA DANSI.
Sasa jamani Tunavaaje Ehh Maswahiba wangu. Akina Dada Mi huko simo. Nimefanikiwa kutafuta baadhi ya picha za wasanii mbalimbali wakiwa katika shughuli kama Hizi za awards.. Kuna Suit huku ndani na mengineyo. Chungulia hapo chini..
Huna SIM Card? Hakuna Tatizo! Kwetu eSIM Inakuwezesha Kuunganishwa Nchi
Zaidi ya 190
-
Fikiria unatua katika nchi mpya na intaneti yako tayari inafanya kazi
kabla hata hujatoka uwanja wa ndege. Hakuna haja ya kutafuta Wi-Fi. Hakuna
kununua...






0 comments:
Post a Comment