Friday, February 18, 2011

CHANGIA WAATHIRIKA WA MABOMU GONGO LA MBOTO


Ni Masikitiko Makubwa na Huzuni pia kwa Wale wote waliopotelewa na ndugu, jamaa na marafiki na pia Wale ambao hawana Makazi ya kuishi kutokana na Ajali ya Kulipuka kwa ghala la jeshi la Silaha Gongo La Mboto.
HILI NI JANGA NA TATIZO LETU WATANZANIA WOTE KAMA MDAU UNA NAFASI KUUBWA YA KUCHANGIA MAAFA HAYA KWA HALI NA MALI KWANI WAHANGA HAWA WANAHITAJI DAWA,DAMU NA VYAKULA

(vinashauriwa vile vikavu kama biscut,mikate nk ambavyo si vya kupika) PIA ZINAHITAJIKA NGUO (mashuka, kanga nk) BILA KUSAHAU PAMBA KWA KINAMAMA

ZIFUATAZO NI NJIA MBALIMBALI ZA KUFIKISHA MCHANGO WAKO:

1. Vodacom Foundation Wamenitoa Namba ya Kutoa Mchango wako. (Red Alert) Tuma meseji yenye neno MAAFA kwenda 15599 kutoka mtandao wowote nchini na utakuwa umechangia Shilingi 1000/- kwa kila sms




2.   Pamoja na kuwawezesha watanzania kutuma mchango wao kupitia ujumbe mfupi, Vodacom Foundation pia unakusanya misaada ya chakula na maji na vifaa mbalimbali katika Ofisi zao zilizopo Mlimani city kwa watu ambao hawajui waipeleke wapi. Misaada hiyo itakabidhiwa kwa red Cross ambao wanahudumia wahanga waliopo Uwanja wa taifa na sehemu mbalimbali


3.  Pia Vodacom foundation imetoa namba za simu kwa timu ya clouds ilioanzisha kituo cha habari na matukio huko shule ya mzambarauni ukonga. Namba hizi zinatumika kupiga bure na kutoa taarifa ya kupotelewa Ndugu au jamaa na pia kutoa taarifa ya maafa zaidi ambayo hayajulikani ili taarifa ziende kwa wahusika. Namba hizi ni 0767 111401 , 0767111402 na 0767111403
 
 

0 comments:

 

JOSE MARA © Copyright 2010 All Rights Reserved . Developed by MTAA KWA MTAA