Friday, July 9, 2010

NYUMA YA PAZIA: SHOOTING YA NYIMBO YANGU MPYA IITWAYO "SHANI"


niko katika maandalizi ya kushoot video ya nyimbo yangu mpya iitwayo "SHANI" ambayo kwa sasa inaonekana katika luninga mbali mbali ila bado haijaanza kusikika redioni lakini si muda mrefu mambo yatakwenda poa na itaanza kusikika pia huko.
mtu mzima nikiwa katika action tofauti tofauti za video ya "SHANI" ambayo inaonekana kupitia luninga mbali mbali .wapenzi wa Josee Mara natumai mmeshaiona na pia mnaendelea kuiona kupitia luninga zenu kwani hii ngoma ni Babkubwa.
nikitafakari kabla sijaendelea kwa hatua nyingine ya action
nikiwa na mwanadada alieigiza kama shani katika wimbo huo wakati wa shooting iliyofanyika katika fukwe ya Mbalamwezi (zamani Malaika) ,jijini Dar
nikiwa na wawezeshaji wa video yangu ya "SHANI" ,Kallaghe Picture's ambao kwa kweli waliifanya kazi hii vizuri sana.alieshika kamera ni John Kallaghe ambaye ndio kiongozi katika libeneke hili.

3 comments:

Anonymous said...

Mjomba speed hiyo mjomba wakimbizeee. Umeamua kaka kazi nzuri.Tunakukubali sana mtu wetu mbunge wetu wa msasani.Mac hapa

Anonymous said...

kazi nzuri shem. Mungu abariki kipaji chako. Tuko nawe sambamba. Hongera Monica kwa kuwa bega kwa bega na mumeo mpenzi. Mungu awape furaha tele katika familia yenu.

Sekisei said...

Jose Mara unatisha.nimefurahia sana kujituma kwako.jamani afadhali wasanii wa muziki wa dansi nao mjitangaze.nakushauri husibague tupe habari za band zote,fm,twanga acudo na nyinginezo.big up kaka sana. na kutakuwa na wanaokukatisha tamaa na macomment ya kipuuzi yapuuze songa mbele tu wewe.

 

JOSE MARA © Copyright 2010 All Rights Reserved . Developed by MTAA KWA MTAA