Thursday, July 22, 2010

Rafiki Yangu Wa Ukweli.


Aisee mi nafahamiana na watu wengi sana. Lakini ninae rafiki yangu mmoja wa ukweli sana. Huwa hatuonani mara kwa mara wala hatu hang out saana pamoja lakini lake langu. Anaitwa Collins Sangija aka Collins USA (Mwenye shati nyeusi ya mistari) Na huyu ndie alikuwa Best Man wangu kwenye harusi.


Nikiwa na Collins kwenye mgahawa wa Samaki samaki pale mlimani City. Kuna wimbo kwenye album yangu nimeimba kwa ajili yake .Hapa tuko na Mtengeneza video kutoka kampuni ya GRM tutakaefanya nae kazi katika songi hilo. STAY TUNED ni Bonge la Rhumba

13 comments:

Anonymous said...

Mzuri. Marital status please

Jose Mara on July 23, 2010 at 1:47 PM said...

Ana mke Mama Vero na watoto watatu. Jose

Anonymous said...

Usitubanie Jose kaoa kweli? Afu mzuri mmefanana kakuzidi urefu.

Anonymous said...

Ameoa nini tunaomba namba he heee. oh na kazi yake nini mana sitaki maskini mie

Anonymous said...

Hivi wanawake wa kibongo mna matatizo gani si mmekwishambiwa ana mke? Kaka afadhali yako ulichagua best man wa mana wengine tulichagua viwembe wakawala wake zetu. Wanawake kama hao wa juu hawapitwi kujiuza uza tu.

Anonymous said...

josee huyu kaka mcongo au mbongo?

Anonymous said...

Wanaume bwana,wao kuuliza dada fulani kwao sawa,ila mkuki wauma pale tunapouliza kaka fulani!kwani ana alama usoni ana Mke?au huyo dada katukana?

Anonymous said...

Jose habari yako? afadhali leo umetuletea picha ya huyu jamaa,namsikia tu mara kwa mara sijapata kumuona,tuletee picha Zake zaidi,mbona nasikia anajua kuvaa sana?naona kawaida...

Anonymous said...

Mh wewe uliesema anafanana na Jose mara una makengeza. Kuvaa anajua sana tu sema msiri sana mambo yake chini chini. nisimwage mchele kwenye kuku wengi

Anonymous said...

Mi namjua sana collins alikuwa huku arusha. ni mbongo.msukuma tena

Anonymous said...

HUO WIMBO UNAMHUSU HUYO SIJUI COLLINS?AU MAISHA YA KILA SIKU?NAONA KUNA LA ZIADA, NI COLLINS TU HAO KINA DADA HAWAULIZI KUHUSU NYIMBO TAMAA ZITAWAUA...TUELEZE KIDOGO KUHUSU HUO WIMBO,ACHANA NA HAO KINA DADA

Anonymous said...

Mtoto wa kimara lete habari!!ebwanae hao GRM si ndio wanaofanya movies hapa bongo?je gharama zao sio kubwa kwa music video?naona kama haitalipa kwa bongo kwa sababu siamini kama muziki unalipa kiasi hicho,nimeona baadhi ya movies walizofanya ziko kwenye ubora unaokubalika,so wasiwasi wangu ni kuhusu gharama zao!

Anonymous said...

Josee huyo mtot white aliyepiga picha na Kalala junior anaitwa nani...maana si mchezo yupo bendi gani.

 

JOSE MARA © Copyright 2010 All Rights Reserved . Developed by MTAA KWA MTAA