Saturday, January 1, 2011

Salamu za Mwaka mpya


Habari wadau. Napenda kuchukua fursa hii kutuma salamu zangu za sikuku ya mwaka mpya kwa wapenzi wote wa Jose Mara Blog,wapenzi wa Jose Mara Kama Msanii,wapenzi wa Jose Mara na Kundi la Mapacha Watatu na bila kusahau wapenzi wote wa FM academia wazee wa Ngwasuma.

Nashukuru mungu katika malengo yangu ya kazi makuu matatu mawili nimeyakamilisha. Nimeweza kumaliza na kuzindua album ya band pamoja na wana Ngwasuma wote. Nimeweza kukamilisha na kuzindua kwa pamoja na Chokoraa na Kalala Junior album ya Mapacha watatu na sasa iko sokoni.
Kilichobaki ni album binafsi ya Jose Mara, hii itakuwa na nafasi yake mwaka 2011 kwa uwezo wake mwenyezi pamoja support yenu mashabiki wangu pamoja tutaweza.

Basi nawatakia heri na fanaka tele kwa mwaka 2011.

Jose Mara.

3 comments:

Anonymous said...

Happy new year to you jose. Pliz uiupdate blog yako tunapenda kujua nini kinaendelea.

Anonymous said...

Asante kila la kheri kwako pia.

Anonymous said...

Mhh hatimie umerudi jose mara wa kimara. Happy new year to you too

 

JOSE MARA © Copyright 2010 All Rights Reserved . Developed by MTAA KWA MTAA